Yeremia 19:10
Jeremiah 19:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kisha livunje lile gudulia wale walio pamoja nawe wakiwa wanaangalia,
Jeremiah 19:10 in English
Jeremiah 19:10 · Berean Standard Bible
Then you are to shatter the jar in the presence of the men who accompany you,
Context
8Nitauharibu mji huu na kuufanya kitu cha kudharauliwa. Wote wapitao karibu watashangaa na kuudhihaki kwa sababu ya majeraha yake yote. 9Nitawafanya wao kula nyama ya wana wao na binti zao; kila mmoja atakula nyama ya mwenzake wakati wa dhiki ya kuzungukwa na jeshi lililowekwa juu yao na adui wanaotafuta uhai wao.’ 10“Kisha livunje lile gudulia wale walio pamoja nawe wakiwa wanaangalia, 11uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: Nitalivunja taifa hili na mji huu kama gudulia hili la mfinyanzi lilivyovunjwa, nalo haliwezi kutengenezeka tena. Watawazika waliokufa huko Tofethi hata isiwepo nafasi zaidi. 12Hivi ndivyo nitakavyopafanya mahali hapa na kwa wale waishio ndani yake, asema Bwana. Nitaufanya mji huu kama Tofethi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.