Yeremia 17:10
Jeremiah 17:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Mimi Bwana huchunguza moyo na kuzijaribu nia, ili kumlipa mtu kwa kadiri ya mwenendo wake, kwa kadiri ya matendo yake yanavyostahili.”
Jeremiah 17:10 in English
Jeremiah 17:10 · Berean Standard Bible
I, the LORD, search the heart; I examine the mind * to reward a man according to his way, by what his deeds deserve.
Context
8Atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji
uenezao mizizi yake karibu na kijito cha maji.
Hauogopi wakati wa joto ujapo;
majani yake ni mabichi daima.
Hauna hofu katika mwaka wa ukame
na hautaacha kuzaa matunda.” 9Moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote,
ni mwovu kupita kiasi.
Ni nani awezaye kuujua? 10“Mimi Bwana huchunguza moyo
na kuzijaribu nia,
ili kumlipa mtu kwa kadiri ya mwenendo wake,
kwa kadiri ya matendo yake yanavyostahili.” 11Kama kware aanguaye mayai asiyoyataga,
ndivyo alivyo mtu apataye mali kwa njia zisizo za haki.
Maisha yake yafikapo katikati, siku zitamwacha,
na mwishoni atabainika kuwa mpumbavu. 12Kiti cha enzi kilichotukuzwa, kilichoinuliwa tangu mwanzo,
ndiyo sehemu yetu ya mahali patakatifu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.