Yeremia 14:22
Jeremiah 14:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Je, kuna sanamu yoyote isiyofaa kitu ya mataifa iwezayo kuleta mvua? Je, anga peke yake zaweza kutoa mvua? La hasha, ni wewe peke yako, Ee Bwana, Mungu wetu. Kwa hiyo tumaini letu liko kwako, kwa kuwa wewe ndiwe ufanyaye haya yote.
Jeremiah 14:22 in English
Jeremiah 14:22 · Berean Standard Bible
Can the worthless idols of the nations bring rain? Do the skies alone send showers? Is this not by You, O LORD our God? So we put our hope in You, for You have done all these things.
Context
20Ee Bwana, tunatambua uovu wetu
na kosa la baba zetu;
kweli tumetenda dhambi dhidi yako. 21Kwa ajili ya jina lako usituchukie kabisa;
usikidharau kiti chako cha enzi kilichotukuka.
Kumbuka agano lako nasi
na usilivunje. 22Je, kuna sanamu yoyote isiyofaa kitu ya mataifa
iwezayo kuleta mvua?
Je, anga peke yake zaweza kutoa mvua?
La hasha, ni wewe peke yako,
Ee Bwana, Mungu wetu.
Kwa hiyo tumaini letu liko kwako,
kwa kuwa wewe ndiwe ufanyaye haya yote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.