Yeremia 11:21
Jeremiah 11:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kwa hiyo hili ndilo Bwana asemalo kuhusu watu wa Anathothi wale wanaotafuta uhai wako wakisema, ‘Usitoe unabii kwa jina la Bwana, la sivyo utakufa kwa mikono yetu’:
Jeremiah 11:21 in English
Jeremiah 11:21 · Berean Standard Bible
Therefore this is what the LORD says concerning the people of Anathoth who are seeking your life and saying, “You must not prophesy in the name of the LORD, or you will die by our hand.”
Context
19Nilikuwa kama mwana-kondoo mpole aliyeongozwa machinjoni; mimi sikutambua kwamba walikuwa wamefanya shauri baya dhidi yangu, wakisema,
“Sisi na tuuangamize mti na matunda yake;
nasi tumkatilie mbali kutoka nchi ya walio hai,
ili jina lake lisikumbukwe tena.” 20Lakini, Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, wewe uhukumuye kwa haki,
nawe uchunguzaye moyo na akili,
wacha nione ukiwalipiza wao kisasi,
kwa maana kwako nimeweka shauri langu. 21“Kwa hiyo hili ndilo Bwana asemalo kuhusu watu wa Anathothi wale wanaotafuta uhai wako wakisema, ‘Usitoe unabii kwa jina la Bwana, la sivyo utakufa kwa mikono yetu’: 22kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nitawaadhibu. Vijana wao waume watakufa kwa upanga, wana wao na binti zao kwa njaa. 23Hawatasaziwa hata mabaki kwao, kwa sababu nitaleta maafa kwa watu wa Anathothi katika mwaka wa adhabu yao.’ ”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.