Yeremia 1:18
Jeremiah 1:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Leo nimekufanya mji wenye ngome, nguzo ya chuma, na ukuta wa shaba ili kusimama dhidi ya nchi yote: dhidi ya wafalme wa Yuda, maafisa wake, makuhani wake na watu wa nchi hiyo.
Jeremiah 1:18 in English
Jeremiah 1:18 · Berean Standard Bible
Now behold, this day I have made you like a fortified city, an iron pillar, and bronze walls against the whole land—against the kings of Judah, its officials, its priests, and the people of the land.
Context
16Nitatoa hukumu zangu kwa watu wangu
kwa sababu ya uovu wao wa kuniacha mimi,
kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine
na kuabudu kile ambacho mikono yao imekitengeneza. 17“Jiandae! Simama useme chochote nitakachokuamuru. Usiwaogope, la sivyo nitakufanya uwaogope wao. 18Leo nimekufanya mji wenye ngome, nguzo ya chuma, na ukuta wa shaba ili kusimama dhidi ya nchi yote: dhidi ya wafalme wa Yuda, maafisa wake, makuhani wake na watu wa nchi hiyo. 19Watapigana nawe lakini hawatakushinda, kwa kuwa niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,” asema Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.