Waamuzi 9:32
Judges 9:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sasa, basi, usiku huu wewe uondoke na watu wako ili mje kuwavizia mashambani.
Judges 9:32 in English
Judges 9:32 · Berean Standard Bible
Now then, tonight you and the people with you are to come and lie in wait in the fields.
Context
30Zebuli aliyekuwa mtawala wa mji aliposikia aliyosema Gaali mwana wa Ebedi, akakasirika sana. 31Akatuma ujumbe uende kwa Abimeleki kwa siri na kusema, “Gaali mwana wa Ebedi na ndugu zake wamekuja Shekemu, na wanauchochea mji huu kinyume chako. 32Sasa, basi, usiku huu wewe uondoke na watu wako ili mje kuwavizia mashambani. 33Kisha asubuhi wakati wa kuchomoza jua, amka mapema na ujipange dhidi ya huo mji. Wakati yeye na jeshi lililo pamoja naye watakapotoka kukabiliana nanyi, mwaweza kuwatendea kwa kadiri mnavyoweza.” 34Kwa hiyo Abimeleki pamoja na jeshi lake lote wakaondoka usiku na kujificha karibu na Shekemu wakiwa vikosi vinne.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.