Waamuzi 7:10
Judges 7:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini kama unaogopa kushambulia, shuka kambini pamoja na mtumishi wako Pura,
Judges 7:10 in English
Judges 7:10 · Berean Standard Bible
But if you are afraid to do so, then go down to the camp with your servant Purah
Context
8Hivyo Gideoni akawaacha wale Waisraeli wengine kila mmoja aende kwenye hema yake. Akabakia na wale 300, ambao walichukua vyakula na tarumbeta za wale wenzao.
Basi kambi ya Wamidiani ilikuwa chini yake bondeni. 9Usiku ule ule Bwana akamwambia Gideoni, “Ondoka, ushuke kambini, kwa kuwa nimeitia mkononi mwako. 10Lakini kama unaogopa kushambulia, shuka kambini pamoja na mtumishi wako Pura, 11nawe sikiliza wanayosema. Hatimaye, utatiwa moyo kushambulia kambi.” Basi yeye na Pura mtumishi wake wakashuka na kufikia walinzi wa mbele wenye silaha waliokuwa mle kambini. 12Wamidiani, Waamaleki na mataifa mengine yote ya mashariki walikaa bondeni, nao walikuwa mfano wa nzige kwa wingi wao. Ngamia zao hazikuhesabika, wingi wao ulikuwa kama mchanga wa ufuoni mwa bahari.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.