Waamuzi 5:12
Judges 5:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
‘Amka, amka! Debora! Amka, amka, uimbe! Ee Baraka! Inuka, chukua mateka wako uliowateka, ee mwana wa Abinoamu.’
Judges 5:12 in English
Judges 5:12 · Berean Standard Bible
‘Awake, awake, O Deborah! Awake, awake, sing a song! Arise, O Barak, and take hold of your captives, O son of Abinoam!’
Context
10“Nanyi mpandao punda weupe,
mkiketi juu ya matandiko ya thamani,
nanyi mtembeao barabarani,
fikirini 11juu ya sauti za waimbaji
mahali pa kunyweshea maji.
Wanasimulia matendo ya haki ya Bwana,
matendo ya haki ya mashujaa wake
katika Israeli.
“Ndipo watu wa Bwana
walipoteremka malangoni pa mji. 12‘Amka, amka! Debora!
Amka, amka, uimbe!
Ee Baraka! Inuka,
chukua mateka wako uliowateka,
ee mwana wa Abinoamu.’ 13“Ndipo mabaki ya watu
wakashuka dhidi ya wenye nguvu,
watu wa Bwana,
wakashuka dhidi ya mashujaa wenye nguvu. 14Kutoka Efraimu wakaja watu, ambao chimbuko lao ni Amaleki;
Benyamini akiwa miongoni
mwa watu waliokufuata.
Kutoka Makiri wakashuka viongozi,
na kutoka Zabuloni wale washikao
fimbo ya jemadari.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.