Waamuzi 20:24
Judges 20:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo Waisraeli wakawakaribia Wabenyamini siku ya pili.
Judges 20:24 in English
Judges 20:24 · Berean Standard Bible
On the second day the Israelites advanced against the Benjamites.
Context
22Lakini Waisraeli wakatiana moyo kila mmoja na mwenzake, nao wakajiweka kwenye nafasi zao katika vile vita mara ya pili mahali pale walipokuwa wamejiweka mara ya kwanza. 23Waisraeli wakapanda mbele za Bwana na kulia mbele zake mpaka jioni, nao wakamuuliza Bwana wakisema, “Je, tupande tena kupigana vita na Wabenyamini, ndugu zetu?”
Bwana akajibu, “Pandeni mkapigane nao.” 24Ndipo Waisraeli wakawakaribia Wabenyamini siku ya pili. 25Wakati huu, Wabenyamini walipotoka Gibea ili kupigana nao, wakawaua watu Waisraeli 18,000, wote wakiwa wamejifunga panga. 26Ndipo Waisraeli, watu wote, wakapanda Betheli, huko wakakaa mbele za Bwana wakilia. Wakafunga siku ile mpaka jioni na kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya amani kwa Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.