Waamuzi 20:14
Judges 20:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakatoka katika miji yao, wakakutanika Gibea ili kupigana na Waisraeli.
Judges 20:14 in English
Judges 20:14 · Berean Standard Bible
And from their cities they came together at Gibeah to go out and fight against the Israelites.
Context
12Makabila ya Israeli yakatuma watu kwenda katika kabila la Benyamini lote na kuwaambia, “Ni uovu gani huu wa kutisha uliotendeka katikati yenu? 13Basi watoeni hao watu waovu kabisa walioko Gibea, ili tupate kuwaua na kuondoa uovu katika Israeli.”
Lakini Wabenyamini hawakuwasikia ndugu zao, Waisraeli. 14Wakatoka katika miji yao, wakakutanika Gibea ili kupigana na Waisraeli. 15Siku ile Wabenyamini wakakusanya watu 26,000 kutoka miji yao, waliojifunga panga, mbali na hao 700 waliochaguliwa miongoni mwa hao waliokaa Gibea. 16Miongoni mwa hao askari wote kulikuwa na watu 700 bora waliochaguliwa watumiao mkono wa kushoto, kila mmoja wao aliweza kutupa jiwe kwa kombeo na kulenga unywele mmoja bila kukosa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.