Waamuzi 16:1
Judges 16:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Siku moja Samsoni alienda Gaza, akamwona mwanamke kahaba, naye akaingia kwake.
Judges 16:1 in English
Judges 16:1 · Berean Standard Bible
One day Samson went to Gaza, where he saw a prostitute and went in to spend the night with her.
Context
1Siku moja Samsoni alienda Gaza, akamwona mwanamke kahaba, naye akaingia kwake. 2Watu wa Gaza wakaambiwa, “Samsoni amekuja huku!” Hivyo wakapazingira mahali pale nao wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji. Wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, “Tumvizie hadi mapambazuko, ndipo tutamuua.” 3Samsoni akalala mpaka usiku wa manane. Akaondoka katikati ya usiku, akashika milango ya lango la mji pamoja na miimo yake miwili, akaingʼoa, makomeo yake na vyote. Akaviweka mabegani mwake na kuvipeleka mpaka kwenye kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.