Waamuzi 15:9
Judges 15:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wafilisti wakapanda na kupiga kambi huko Yuda na kuenea huko Lehi.
Judges 15:9 in English
Judges 15:9 · Berean Standard Bible
Then the Philistines went up, camped in Judah, and deployed themselves near the town of Lehi.*
Context
7Samsoni akawaambia, “Kwa kuwa mmetenda hivyo, hakika sitatulia mpaka niwe nimelipiza kisasi juu yenu.” 8Akawashambulia kwa ukali kwa mapigo makuu na kuwaua watu wengi sana. Kisha akateremka na kukaa katika ufa kwenye mwamba wa Etamu. 9Wafilisti wakapanda na kupiga kambi huko Yuda na kuenea huko Lehi. 10Watu wa Yuda wakawauliza, “Kwa nini mmekuja kupigana nasi?”
Wakawajibu, “Tumekuja ili kumkamata Samsoni na kumtenda kama alivyotutendea.” 11Ndipo watu 3,000 toka Yuda walipoteremka na kwenda kwenye ufa wa mwamba huko Etamu, na kumwambia Samsoni, “Je, hujatambua kuwa Wafilisti wanatutawala? Ni nini hiki ulichotutendea?”
Akawajibu, “Mimi nimewatendea tu kile walichonitendea.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.