Waamuzi 15:12
Judges 15:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakamwambia, “Tumekuja kukufunga na kukutia mikononi mwa Wafilisti.” Samsoni akawaambia, “Niapieni kuwa hamtaniua ninyi wenyewe.”
Judges 15:12 in English
Judges 15:12 · Berean Standard Bible
But they said to him, “We have come down to arrest you and hand you over to the Philistines.” Samson replied, “Swear to me that you will not kill me yourselves.”
Context
10Watu wa Yuda wakawauliza, “Kwa nini mmekuja kupigana nasi?”
Wakawajibu, “Tumekuja ili kumkamata Samsoni na kumtenda kama alivyotutendea.” 11Ndipo watu 3,000 toka Yuda walipoteremka na kwenda kwenye ufa wa mwamba huko Etamu, na kumwambia Samsoni, “Je, hujatambua kuwa Wafilisti wanatutawala? Ni nini hiki ulichotutendea?”
Akawajibu, “Mimi nimewatendea tu kile walichonitendea.” 12Wakamwambia, “Tumekuja kukufunga na kukutia mikononi mwa Wafilisti.”
Samsoni akawaambia, “Niapieni kuwa hamtaniua ninyi wenyewe.” 13Wakamjibu, “Sisi hatutakuua, bali tutakufunga tu na kukutia mikononi mwao.” Basi wakamfunga kwa kamba mbili mpya. Wakamchukua toka huko kwenye ufa katika mwamba. 14Alipokaribia Lehi, Wafilisti wakamjia wakipiga kelele. Roho wa Bwana akamjia juu yake kwa nguvu. Kamba zilizomfunga mikono yake zikawa kama kitani iliyochomwa kwa moto, na vifungo vyake vikaanguka chini toka mikononi mwake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.