Waamuzi 14:7
Judges 14:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi akateremka na kuongea na yule mwanamke, naye akampendeza Samsoni.
Judges 14:7 in English
Judges 14:7 · Berean Standard Bible
Then Samson continued on his way down and spoke to the woman, because she was pleasing to his eyes.
Context
5Samsoni akateremkia Timna pamoja na baba yake na mama yake. Walipofika kwenye mashamba ya mizabibu huko Timna, ghafula mwana simba akamjia akimngurumia. 6Roho wa Bwana akaja juu yake kwa nguvu, naye akampasua yule simba kwa mikono yake bila silaha yoyote kama vile mtu ampasuavyo mwana-mbuzi, wala hakumwambia baba yake wala mama yake aliyoyafanya. 7Basi akateremka na kuongea na yule mwanamke, naye akampendeza Samsoni. 8Baada ya muda aliporudi ili akamwoe, akatazama kando ili kuutazama mzoga wa yule simba, na tazama, kulikuwa na kundi la nyuki ndani ya ule mzoga wa simba na kulikuwa na asali; 9akachukua asali mkononi mwake akaendelea huku akila. Alipowafikia baba yake na mama yake, akawapa ile asali nao wakala. Lakini hakuwaambia kuwa alitwaa asali kutoka kwenye mzoga wa simba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.