Native Bible

Isaiah 7:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndipo Bwana akamwambia Isaya, “Toka uende, wewe na mwanao Shear-Yashubu,* mkutane na Ahazi huko mwisho wa mfereji wa Bwawa la Juu, kwenye barabara iendayo Shamba la Dobi.

Isaiah 7:3 in English

Isaiah 7:3 · Berean Standard Bible

Then the LORD said to Isaiah, “Go out with your son Shear-jashub * to meet Ahaz at the end of the aqueduct that feeds the upper pool, on the road to the Launderer’s Field,

Context

1Wakati Ahazi mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, alipokuwa mfalme wa Yuda, Mfalme Resini wa Aramu,* na Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli walipanda kupigana dhidi ya Yerusalemu, lakini hawakuweza kuushinda. 2Wakati huu nyumba ya Daudi iliambiwa, “Aramu wameungana na Efraimu.” Kwa hiyo mioyo ya Ahazi na watu wake ilitikiswa, kama miti ya msituni inavyotikiswa na upepo. 3Ndipo Bwana akamwambia Isaya, “Toka uende, wewe na mwanao Shear-Yashubu,* mkutane na Ahazi huko mwisho wa mfereji wa Bwawa la Juu, kwenye barabara iendayo Shamba la Dobi. 4Mwambie, ‘Uwe mwangalifu, utulie na usiogope. Usife moyo kwa ajili ya watu hawa wawili walio kama visiki vya kuni vifukavyo moshi, kwa ajili ya hasira kali ya Resini na Aramu na ya mwana wa Remalia. 5Aramu, Efraimu na mwana wa Remalia wamepanga shauri baya ili wakuangamize, wakisema,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.