Isaya 66:3
Isaiah 66:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali ni kama yeye auaye mtu, na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo, ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa. Yeyote atoaye sadaka ya nafaka, ni kama yule aletaye damu ya nguruwe, na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu, ni kama yule aabuduye sanamu. Wamejichagulia njia zao wenyewe, nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao.
Isaiah 66:3 in English
Isaiah 66:3 · Berean Standard Bible
Whoever slaughters an ox is like one who slays a man; whoever sacrifices a lamb is like one who breaks a dog’s neck; whoever presents a grain offering is like one who offers pig’s blood; whoever offers frankincense is like one who blesses an idol. Indeed, they have chosen their own ways and delighted in their abominations.
Context
1Hili ndilo asemalo Bwana,
“Mbingu ni kiti changu cha enzi,
nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu.
Iko wapi nyumba mtakayoijenga kwa ajili yangu?
Mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi? 2Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote,
hivyo vikapata kuwepo?”
asema Bwana.
“Mtu huyu ndiye ninayemthamini:
yeye ambaye ni mnyenyekevu
na mwenye roho yenye toba,
atetemekaye asikiapo neno langu. 3Lakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali
ni kama yeye auaye mtu,
na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo,
ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa.
Yeyote atoaye sadaka ya nafaka,
ni kama yule aletaye damu ya nguruwe,
na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu,
ni kama yule aabuduye sanamu.
Wamejichagulia njia zao wenyewe,
nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao. 4Hivyo, mimi pia nitawachagulia mapigo makali,
nami nitaleta juu yao kile wanachokiogopa.
Kwa maana nilipoita, hakuna yeyote aliyejibu,
niliposema, hakuna yeyote aliyesikiliza.
Walifanya maovu machoni pangu
na kuchagua lile linalonichukiza.” 5Sikieni neno la Bwana,
ninyi mtetemekao kwa neno lake:
“Ndugu zenu wanaowachukia ninyi
na kuwatenga ninyi kwa sababu ya Jina langu, wamesema,
‘Bwana na atukuzwe,
ili tupate kuona furaha yenu!’
Hata sasa wataaibika.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.