Native Bible

Isaiah 63:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa nini mavazi yako ni mekundu, kama ya yule akanyagaye shinikizo la zabibu?

Isaiah 63:2 in English

Isaiah 63:2 · Berean Standard Bible

Why are Your clothes red, and Your garments like one who treads the winepress?

Context

1Ni nani huyu anayekuja kutoka Edomu, kutoka Bosra, mwenye mavazi yaliyotiwa madoa mekundu? Ni nani huyu, aliyevikwa joho la kifahari, anayetembea kwa ukuu wa nguvu zake? “Mimi ndimi, nisemaye katika haki, mwenye nguvu wa kuokoa.” 2Kwa nini mavazi yako ni mekundu, kama ya yule akanyagaye shinikizo la zabibu? 3“Nimekanyaga shinikizo la zabibu peke yangu; kutoka mataifa hakuna mtu aliyekuwa pamoja nami. Nimewaponda kwa miguu katika hasira yangu na kuwakanyaga chini katika ghadhabu yangu; damu yao ilitia matone kwenye mavazi yangu, na kutia madoa nguo zangu zote. 4Kwa kuwa siku ya kisasi ilikuwa moyoni mwangu, mwaka wa ukombozi wangu umefika.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.