Isaya 61:11
Isaiah 61:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana kama vile ardhi ifanyavyo chipukizi kuota, na bustani isababishavyo mbegu kuota, ndivyo Bwana Mwenyezi atafanya haki na sifa zichipuke mbele ya mataifa yote.
Isaiah 61:11 in English
Isaiah 61:11 · Berean Standard Bible
For as the earth brings forth its growth, and as a garden enables seed to spring up, so the Lord GOD will cause righteousness and praise to spring up before all the nations.
Context
9Wazao wao watajulikana miongoni mwa mataifa,
na uzao wao miongoni mwa kabila za watu.
Wale wote watakaowaona watatambua
kuwa ni taifa ambalo Bwana amelibariki.” 10Ninafurahia sana katika Bwana,
nafsi yangu inashangilia katika Mungu wangu.
Kwa maana amenivika mavazi ya wokovu,
na kunipamba kwa joho la haki,
kama vile bwana arusi apambavyo
kichwa chake kama kuhani,
na kama bibi arusi ajipambavyo
kwa vito vyake vya thamani. 11Kwa maana kama vile ardhi ifanyavyo chipukizi kuota,
na bustani isababishavyo mbegu kuota,
ndivyo Bwana Mwenyezi atafanya haki na sifa
zichipuke mbele ya mataifa yote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.