Isaya 6:13
Isaiah 6:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hata kama sehemu ya kumi ya watu watabaki katika nchi, itaharibiwa tena. Lakini kama vile mvinje na mwaloni ibakizavyo visiki inapokatwa, ndivyo mbegu takatifu itakavyokuwa kisiki katika nchi.”
Isaiah 6:13 in English
Isaiah 6:13 · Berean Standard Bible
And though a tenth remains in the land, it will be burned again. As the terebinth and oak leave stumps when felled, so the holy seed will be a stump in the land.”
Context
11Ndipo nikasema, “Hadi lini, Ee Bwana?”
Naye akanijibu:
“Hadi miji iwe imeachwa magofu
na bila wakazi,
hadi nyumba zitakapobaki bila watu,
na mashamba yatakapoharibiwa na kuangamizwa, 12hadi Bwana atakapokuwa amekwisha kumpeleka kila mmoja mbali sana,
na nchi itakapokuwa imeachwa kabisa. 13Hata kama sehemu ya kumi ya watu watabaki katika nchi,
itaharibiwa tena.
Lakini kama vile mvinje na mwaloni
ibakizavyo visiki inapokatwa,
ndivyo mbegu takatifu
itakavyokuwa kisiki katika nchi.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.