Isaya 59:20
Isaiah 59:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Mkombozi atakuja Sayuni, kwa wale wa Yakobo wanaozitubu dhambi zao,” asema Bwana.
Isaiah 59:20 in English
Isaiah 59:20 · Berean Standard Bible
“The Redeemer will come to Zion, to those in Jacob who turn from transgression,*” declares the LORD.
Context
18Kulingana na kile walichokuwa wametenda,
ndivyo atakavyolipa
ghadhabu kwa watesi wake
na kisasi kwa adui zake,
atavilipa visiwa sawa na wanavyostahili. 19Kuanzia magharibi, watu wataliogopa jina la Bwana
na kuanzia mawio ya jua, watauheshimu utukufu wake.
Wakati adui atakapokuja kama mafuriko,
Roho wa Bwana atainua kiwango dhidi yake na kumshinda. 20“Mkombozi atakuja Sayuni,
kwa wale wa Yakobo
wanaozitubu dhambi zao,”
asema Bwana. 21“Kwa habari yangu mimi, hili ndilo agano langu nao,” asema Bwana. “Roho wangu, aliye juu yenu, na maneno yangu ambayo nimeyaweka katika vinywa vyenu, havitaondoka vinywani mwenu, wala kutoka vinywani mwa watoto wenu, wala kutoka vinywani mwa wazao wao, kuanzia sasa na hata milele,” asema Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.