Isaya 57:11
Isaiah 57:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Ni nani uliyemhofu hivyo na kumwogopa hata ukawa mwongo kwangu, wala hukunikumbuka au kutafakari hili moyoni mwako? Si ni kwa sababu nimekuwa kimya muda mrefu hata huniogopi?
Isaiah 57:11 in English
Isaiah 57:11 · Berean Standard Bible
Whom have you dreaded and feared, so that you lied and failed to remember Me or take this to heart? Is it not because I have long been silent that you do not fear Me?
Context
9Ulikwenda kwa Moleki* ukiwa na mafuta ya zeituni,
na ukaongeza manukato yako.
Ukawatuma wajumbe wako mbali sana,
ukashuka kwenye kaburi* lenyewe! 10Ulikuwa umechoshwa na njia zako zote,
lakini hukusema, ‘Hakuna tumaini.’
Ulipata uhuisho wa nguvu zako,
kwa sababu hiyo hukuzimia. 11“Ni nani uliyemhofu hivyo na kumwogopa
hata ukawa mwongo kwangu,
wala hukunikumbuka
au kutafakari hili moyoni mwako?
Si ni kwa sababu nimekuwa kimya muda mrefu
hata huniogopi? 12Nitaifunua haki yako na matendo yako,
nayo hayatakufaidi. 13Utakapolia kwa kuhitaji msaada,
sanamu zako ulizojikusanyia na zikuokoe!
Upepo utazipeperusha zote,
pumzi peke yake itazipeperusha,
Lakini mtu atakayenifanya kimbilio lake,
atairithi nchi
na kuumiliki mlima wangu mtakatifu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.