Isaya 5:6
Isaiah 5:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitalifanya nchi ya ukiwa isiyokaliwa na watu, halitakatiwa matawi wala kulimwa, nayo michongoma na miiba itamea huko, nitaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.”
Isaiah 5:6 in English
Isaiah 5:6 · Berean Standard Bible
I will make it a wasteland, neither pruned nor cultivated, and thorns and briers will grow up. I will command the clouds that rain shall not fall on it.”
Context
4Ni nini zaidi ambacho kingeweza kufanyika kwa shamba langu la mizabibu
kuliko yale niliyofanya?
Nilipotazamia kupata zabibu nzuri,
kwa nini lilizaa zabibu mbaya tu? 5Sasa nitawaambia lile nitakalolitendea
shamba langu la mizabibu:
Nitaondoa uzio wake,
nalo litaharibiwa,
nitabomoa ukuta wake,
nalo litakanyagwa. 6Nitalifanya nchi ya ukiwa isiyokaliwa na watu,
halitakatiwa matawi wala kulimwa,
nayo michongoma na miiba itamea huko,
nitaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.” 7Shamba la mzabibu la Bwana Mwenye Nguvu Zote
ni nyumba ya Israeli,
na watu wa Yuda
ni bustani yake ya kumpendeza.
Alitazamia haki, lakini akaona umwagaji damu,
alitazamia uadilifu, lakini akasikia vilio vya taabu. 8Ole wenu mnaoongeza nyumba baada ya nyumba
na kuunganisha mashamba baada ya mashamba
hadi hakuna nafasi iliyobaki,
nanyi mnaishi peke yenu katika nchi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.