Isaya 47:8
Isaiah 47:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Sasa basi, sikiliza, ewe kiumbe mpenda anasa, ukaaye mahali pako pa salama, na kujiambia mwenyewe, ‘Mimi ndiye, wala hakuna mwingine zaidi yangu. Kamwe sitakuwa mjane, wala sitafiwa na watoto.’
Isaiah 47:8 in English
Isaiah 47:8 · Berean Standard Bible
So now hear this, O lover of luxury who sits securely, who says to herself, ‘I am, and there is none besides me. I will never be a widow or know the loss of children.’
Context
6Niliwakasirikia watu wangu
na kuaibisha urithi wangu;
niliwatia mikononi mwako,
nawe hukuwaonea huruma.
Hata juu ya wazee
uliweka nira nzito sana. 7Ukasema, ‘Nitaendelea
kuwa malkia milele!’
Lakini hukutafakari mambo haya
wala hukuwaza juu ya kile kingeweza kutokea. 8“Sasa basi, sikiliza, ewe kiumbe mpenda anasa,
ukaaye mahali pako pa salama,
na kujiambia mwenyewe,
‘Mimi ndiye, wala hakuna mwingine zaidi yangu.
Kamwe sitakuwa mjane,
wala sitafiwa na watoto.’ 9Haya mawili yatakupata, kufumba na kufumbua,
katika siku moja:
kufiwa na watoto, na ujane.
Yote yatakupata kwa kipimo kikamilifu,
ijapokuwa uchawi wako ni mwingi,
na uaguzi wako ni mwingi. 10Umeutegemea uovu wako,
nawe umesema, ‘Hakuna yeyote anionaye.’
Hekima yako na maarifa yako vinakupoteza
unapojiambia mwenyewe,
‘Mimi ndiye, wala hakuna mwingine zaidi yangu.’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.