Native Bible

Isaiah 42:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hatapaza sauti wala kupiga kelele, wala hataiinua sauti yake barabarani.

Isaiah 42:2 in English

Isaiah 42:2 · Berean Standard Bible

He will not cry out or raise His voice, nor make His voice heard in the streets.

Context

1“Huyu hapa mtumishi wangu, ninayemtegemeza, mteule wangu, ambaye ninapendezwa naye; nitaweka Roho yangu juu yake, naye ataleta haki kwa mataifa. 2Hatapaza sauti wala kupiga kelele, wala hataiinua sauti yake barabarani. 3Mwanzi uliopondeka hatauvunja, na utambi unaofuka moshi hatauzima. Kwa uaminifu ataleta haki, 4hatazimia roho wala kukata tamaa, mpaka atakaposimamisha haki juu ya dunia. Visiwa vitaweka tumaini lao katika sheria yake.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.