Isaya 40:6
Isaiah 40:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sauti husema, “Piga kelele.” Nami nikasema, “Nipige kelele gani?” “Wanadamu wote ni kama majani, nao utukufu wao wote ni kama maua ya kondeni.
Isaiah 40:6 in English
Isaiah 40:6 · Berean Standard Bible
A voice says, “Cry out!” And I asked, “What should I cry out?” “All flesh is like grass, and all its glory like the flowers of the field.
Context
4Kila bonde litainuliwa,
kila mlima na kilima kitashushwa;
penye mabonde patanyooshwa,
napo palipoparuza patasawazishwa. 5Utukufu wa Bwana utafunuliwa,
nao wanadamu wote watauona pamoja.
Kwa maana kinywa cha Bwana kimenena.” 6Sauti husema, “Piga kelele.”
Nami nikasema, “Nipige kelele gani?”
“Wanadamu wote ni kama majani,
nao utukufu wao wote
ni kama maua ya kondeni. 7Majani hunyauka na maua huanguka,
kwa sababu pumzi ya Bwana huyapuliza.
Hakika wanadamu ni majani. 8Majani hunyauka na maua huanguka,
lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.