Isaya 38:18
Isaiah 38:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana kaburi* haliwezi kukusifu, mauti haiwezi kuimba sifa zako; wale washukao chini shimoni hawawezi kuutarajia uaminifu wako.
Isaiah 38:18 in English
Isaiah 38:18 · Berean Standard Bible
For Sheol cannot thank You; Death cannot praise You. Those who descend to the Pit cannot hope for Your faithfulness.
Context
16Bwana, kwa mambo kama haya watu huishi,
nayo roho yangu hupata uzima katika hayo pia.
Uliniponya
na kuniacha niishi. 17Hakika ilikuwa ya faida yangu
ndiyo maana nikapata maumivu makali.
Katika upendo wako ukaniokoa
kutoka shimo la uharibifu;
umeziweka dhambi zangu zote
nyuma yako. 18Kwa maana kaburi* haliwezi kukusifu,
mauti haiwezi kuimba sifa zako;
wale washukao chini shimoni
hawawezi kuutarajia uaminifu wako. 19Walio hai, walio hai: hao wanakusifu,
kama ninavyofanya leo.
Baba huwaambia watoto wao
habari za uaminifu wako. 20Bwana ataniokoa,
nasi tutaimba kwa vyombo vya nyuzi
siku zote za maisha yetu
katika Hekalu la Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.