Isaya 26:11
Isaiah 26:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ee Bwana, mkono wako umeinuliwa juu, lakini hawauoni. Wao na waone wivu wako kwa ajili ya watu wako tena waaibishwe, moto uliowekwa akiba kwa ajili ya adui zako na uwateketeze.
Isaiah 26:11 in English
Isaiah 26:11 · Berean Standard Bible
O LORD, Your hand is upraised, but they do not see it. They will see Your zeal for Your people and be put to shame. The fire set for Your enemies will consume them!
Context
9Nafsi yangu yakutamani wakati wa usiku,
wakati wa asubuhi roho yangu yakuonea shauku.
Wakati hukumu zako zinapokuja juu ya dunia,
watu wa ulimwengu hujifunza haki. 10Ingawa neema yaonyeshwa kwa waovu,
hawajifunzi haki,
hata katika nchi ya unyofu huendelea kutenda mabaya
wala hawazingatii utukufu wa Bwana. 11Ee Bwana, mkono wako umeinuliwa juu,
lakini hawauoni.
Wao na waone wivu wako kwa ajili ya watu wako tena waaibishwe,
moto uliowekwa akiba kwa ajili ya adui zako na uwateketeze. 12Bwana, unaamuru amani kwa ajili yetu,
yale yote tuliyoweza kuyakamilisha ni wewe uliyetenda kwa ajili yetu. 13Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametutawala,
lakini jina lako pekee ndilo tunaloliheshimu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.