Isaya 25:9
Isaiah 25:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika siku ile watasema, “Hakika huyu ndiye Mungu wetu; tulimtumaini, naye akatuokoa. Huyu ndiye Bwana, tuliyemtumaini; sisi tushangilie na kufurahia katika wokovu wake.”
Isaiah 25:9 in English
Isaiah 25:9 · Berean Standard Bible
And in that day it will be said, “Surely this is our God; we have waited for Him, and He has saved us. This is the LORD for whom we have waited. Let us rejoice and be glad in His salvation.”
Context
7Juu ya mlima huu ataharibu
sitara ihifadhiyo mataifa yote,
kile kifuniko kifunikacho mataifa yote, 8yeye atameza mauti milele.
Bwana Mwenyezi atafuta machozi katika nyuso zote;
ataondoa aibu ya watu wake duniani kote.
Bwana amesema hili. 9Katika siku ile watasema,
“Hakika huyu ndiye Mungu wetu;
tulimtumaini, naye akatuokoa.
Huyu ndiye Bwana, tuliyemtumaini;
sisi tushangilie na kufurahia katika wokovu wake.” 10Mkono wa Bwana utatulia juu ya mlima huu,
bali Moabu atakanyagwa chini
kama majani makavu yakanyagwavyo kwenye shimo la mbolea. 11Watakunjua mikono yao katikati yake,
kama vile mwogeleaji akunjuavyo mikono yake ili aogelee.
Mungu atashusha kiburi chao
licha ya ujanja wa mikono yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.