Isaya 10:2
Isaiah 10:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
kuwanyima maskini haki zao na kuzuilia haki za watu wangu walioonewa, kuwafanya wajane mawindo yao na kuwanyangʼanya yatima.
Isaiah 10:2 in English
Isaiah 10:2 · Berean Standard Bible
to deprive the poor of fair treatment and withhold justice from the oppressed of My people, to make widows their prey and orphans their plunder.
Context
1Ole wao wawekao sheria zisizo za haki,
kwa wale watoao amri za kuonea, 2kuwanyima maskini haki zao
na kuzuilia haki za watu wangu walioonewa,
kuwafanya wajane mawindo yao
na kuwanyangʼanya yatima. 3Mtafanya nini siku ya kutoa hesabu,
wakati maafa yatakapokuja kutoka mbali?
Mtamkimbilia nani awape msaada?
Mtaacha wapi mali zenu? 4Hakutasalia kitu chochote,
isipokuwa kujikunyata miongoni mwa mateka,
au kuanguka miongoni mwa waliouawa.
Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,
mkono wake bado umeinuliwa juu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.