Hosea 9:1
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Usifurahie, ee Israeli; usishangilie kama mataifa mengine. Kwa kuwa hukuwa mwaminifu kwa Mungu wako; umependa ujira wa kahaba kwenye kila sakafu ya kupuria nafaka.
Hosea 9:1 in English
Hosea 9:1 · Berean Standard Bible
Do not rejoice, O Israel, with exultation like the nations, for you have played the harlot against your God; you have made love for hire on every threshing floor.
Context
1Usifurahie, ee Israeli;
usishangilie kama mataifa mengine.
Kwa kuwa hukuwa
mwaminifu kwa Mungu wako;
umependa ujira wa kahaba kwenye kila sakafu
ya kupuria nafaka. 2Sakafu za kupuria nafaka na mashinikizo ya kukamulia divai
havitalisha watu,
divai mpya itawapungukia. 3Hawataishi katika nchi ya Bwana,
Efraimu atarudi Misri
na atakula chakula
kilicho najisi huko Ashuru.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.