Waebrania 11:36
Hebrews 11:36 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wengine walidhihakiwa na kupigwa, hata walifungwa minyororo na kutiwa gerezani.
Hebrews 11:36 in English
Hebrews 11:36 · Berean Standard Bible
Still others endured mocking and flogging, and even chains and imprisonment.
Context
34wakazima makali ya miali ya moto, na wakaepuka kuuawa kwa upanga; udhaifu wao uligeuka kuwa nguvu; pia walikuwa hodari vitani na kuyafukuza majeshi ya wageni. 35Wanawake walipokea watu wao waliokuwa wamekufa, wakafufuliwa. Lakini wengine waliteswa, nao wakakataa kufunguliwa, ili wapate ufufuo ulio bora zaidi. 36Wengine walidhihakiwa na kupigwa, hata walifungwa minyororo na kutiwa gerezani. 37Walipigwa kwa mawe; walipasuliwa vipande viwili kwa msumeno; waliuawa kwa upanga. Walizungukazunguka wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na mbuzi, wakiwa maskini, wakiteswa na kutendwa mabaya, 38watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao. Walizunguka majangwani na milimani, katika mapango na katika mahandaki ardhini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.