Waebrania 11:20
Hebrews 11:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa imani Isaki alimbariki Yakobo na Esau kuhusu maisha yao ya baadaye.
Hebrews 11:20 in English
Hebrews 11:20 · Berean Standard Bible
By faith Isaac blessed Jacob and Esau concerning the future.
Context
18Ingawa Mungu alikuwa amemwambia Abrahamu, “Uzao wako utahesabiwa kupitia kwa Isaki,” 19Abrahamu alihesabu kuwa Mungu angaliweza kumfufua Isaki kutoka kwa wafu. Na kwa kusema kwa mfano, alimpata tena Isaki kutoka kwa wafu. 20Kwa imani Isaki alimbariki Yakobo na Esau kuhusu maisha yao ya baadaye. 21Kwa imani Yakobo alipokuwa anakufa, alimbariki kila mmoja wa mtoto wa Yosefu, akamwabudu Mungu akiwa ameegemea juu ya kichwa cha fimbo yake. 22Kwa imani, Yosefu alipokaribia mwisho wa maisha yake, alinena habari za kutoka kwa wana wa Israeli huko Misri na akatoa maagizo kuhusu mifupa yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.