Hagai 1:12
Haggai 1:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha Zerubabeli mwana wa Shealtieli, Yoshua kuhani mkuu mwana wa Yehosadaki, pamoja na mabaki yote ya watu wakaitii sauti ya Bwana Mungu wao pamoja na ujumbe wa nabii Hagai, kwa sababu alikuwa ametumwa na Bwana Mungu wao. Watu walimwogopa Bwana.
Haggai 1:12 in English
Haggai 1:12 · Berean Standard Bible
Then Zerubbabel son of Shealtiel and Joshua son of Jehozadak, the high priest, as well as all the remnant of the people, obeyed the voice of the LORD their God and the words of the prophet Haggai, because the LORD their God had sent him. So the people feared the LORD.
Context
10Kwa hiyo, kwa sababu yenu mbingu zimezuia umande wake na ardhi mavuno yake. 11Niliita ukame mashambani na milimani, kwenye nafaka, mvinyo mpya, mafuta pamoja na chochote kinachozalishwa na ardhi, juu ya watu na ngʼombe, pamoja na kazi za mikono yenu.” 12Kisha Zerubabeli mwana wa Shealtieli, Yoshua kuhani mkuu mwana wa Yehosadaki, pamoja na mabaki yote ya watu wakaitii sauti ya Bwana Mungu wao pamoja na ujumbe wa nabii Hagai, kwa sababu alikuwa ametumwa na Bwana Mungu wao. Watu walimwogopa Bwana. 13Kisha Hagai, mjumbe wa Bwana, akawapa watu ujumbe huu wa Bwana: “Mimi niko pamoja nanyi,” asema Bwana. 14Kwa hiyo Bwana akachochea roho ya Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, pamoja na roho za mabaki yote ya watu. Walikuja wakaanza kufanya kazi katika nyumba ya Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wao,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.