Mwanzo 9:4
Genesis 9:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Lakini kamwe msile nyama ambayo bado ina damu ya uhai wake, kwa maana damu ni uhai.
Genesis 9:4 in English
Genesis 9:4 · Berean Standard Bible
But you must not eat meat with its lifeblood still in it.
Context
2Wanyama wote wa duniani, ndege wote wa angani, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi, na samaki wote wa baharini wamekabidhiwa mikononi mwenu, nao watawaogopa na kuwahofu. 3Kila kitu chenye uhai kiendacho kitakuwa chakula chenu. Kama vile nilivyowapa mimea mbalimbali, sasa nawapa kila kitu. 4“Lakini kamwe msile nyama ambayo bado ina damu ya uhai wake, kwa maana damu ni uhai. 5Hakika damu ya uhai wenu nitaidai. Nitaidai kutoka kwa kila mnyama. Kutoka kwa kila mwanadamu pia nitaidai kwa ajili ya uhai wa mtu mwenzake. 6“Yeyote amwagaye damu ya mwanadamu,
damu yake itamwagwa na mwanadamu,
kwa kuwa katika mfano wa Mungu,
Mungu alimuumba mwanadamu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.