Mwanzo 50:6
Genesis 50:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Farao akasema, “Panda, uende kumzika baba yako, kama alivyokuapiza kufanya.”
Genesis 50:6 in English
Genesis 50:6 · Berean Standard Bible
Pharaoh replied, “Go up and bury your father, as he made you swear to do.”
Context
4Siku za kumwombolezea zilipokwisha, Yosefu akawaambia washauri wa Farao, “Kama nimepata kibali machoni penu semeni na Farao kwa ajili yangu. Mwambieni, 5‘Baba yangu aliniapisha na kuniambia, “Mimi niko karibu kufa; unizike katika kaburi lile nililochimba kwa ajili yangu mwenyewe katika nchi ya Kanaani.” Sasa nakuomba uniruhusu niende kumzika baba yangu, nami nitarudi.’ ” 6Farao akasema, “Panda, uende kumzika baba yako, kama alivyokuapiza kufanya.” 7Hivyo Yosefu akapanda kwenda kumzika baba yake. Maafisa wote wa Farao wakaenda pamoja naye, watu mashuhuri wa baraza lake na watu mashuhuri wote wa Misri. 8Hawa ni mbali na watu wote wa nyumbani kwa Yosefu, na ndugu zake, na wale wote wa nyumbani mwa baba yake. Ni watoto wao, makundi yao ya kondoo, mbuzi na ngʼombe tu waliobakia katika nchi ya Gosheni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.