Mwanzo 49:10
Genesis 49:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda, wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake, hadi aje yeye ambaye milki ni yake, ambaye utii wa mataifa ni wake.
Genesis 49:10 in English
Genesis 49:10 · Berean Standard Bible
The scepter will not depart from Judah, nor the staff from between his feet,* until Shiloh * comes and the allegiance of the nations is his.
Context
8“Yuda, ndugu zako watakusifu;
mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako;
wana wa baba yako watakusujudia. 9Ee Yuda, wewe ni mwana simba;
unarudi toka mawindoni, mwanangu.
Kama simba hunyemelea na kulala chini,
kama simba jike: nani athubutuye kumwamsha? 10Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda,
wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake,
hadi aje yeye ambaye milki ni yake,
ambaye utii wa mataifa ni wake. 11Atamfunga punda wake katika mzabibu,
naye mwana-punda wake kwenye tawi lililo bora zaidi;
atafua mavazi yake katika divai,
majoho yake katika damu ya mizabibu. 12Macho yake yatakuwa mekundu kwa divai,
meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.