Native Bible

Genesis 47:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yakobo akaishi Misri miaka kumi na saba, nayo miaka ya maisha yake ilikuwa 147.

Genesis 47:28 in English

Genesis 47:28 · Berean Standard Bible

And Jacob lived in the land of Egypt seventeen years, and the length of his life was 147 years.

Context

26Basi Yosefu akaiweka iwe sheria kuhusu nchi ya Misri, ambayo inatumika mpaka leo, kwamba, sehemu ya tano ya mazao ni mali ya Farao. Ni nchi ya makuhani tu ambayo haikuwa ya Farao. 27Basi Waisraeli wakaishi Misri katika nchi ya Gosheni. Wakapata mali huko wakastawi na kuongezeka kwa wingi sana. 28Yakobo akaishi Misri miaka kumi na saba, nayo miaka ya maisha yake ilikuwa 147. 29Wakati ulipokaribia wa Israeli kufa, akamwita mwanawe Yosefu na kumwambia, “Kama nimepata kibali machoni pake, weka mkono wako chini ya paja langu na uniahidi kuwa utanifanyia fadhili na uaminifu. Usinizike Misri, 30lakini nitakapopumzika na baba zangu, unichukue kutoka Misri, ukanizike walipozikwa.” Yosefu akamwambia, “Nitafanya kama unavyosema.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.