Mwanzo 47:2
Genesis 47:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akachagua ndugu zake watano na kuwaonyesha kwa Farao.
Genesis 47:2 in English
Genesis 47:2 · Berean Standard Bible
And he chose five of his brothers and presented them before Pharaoh.
Context
1Yosefu akaenda na kumwambia Farao, “Baba yangu na ndugu zangu wamekuja kutoka nchi ya Kanaani wakiwa na makundi yao ya kondoo, mbuzi na ngʼombe, pamoja na kila kitu walicho nacho, nao sasa wapo huko Gosheni.” 2Akachagua ndugu zake watano na kuwaonyesha kwa Farao. 3Farao akawauliza hao ndugu zake, “Kazi yenu ni nini?”
Wakamjibu, “Watumishi wako ni wachunga mifugo, kama vile baba zetu walivyokuwa.” 4Pia wakamwambia Farao, “Tumekuja kukaa huku kwa muda mfupi, kwa sababu njaa ni kali huko Kanaani, na mifugo ya watumishi wako haina malisho. Kwa hiyo sasa, tafadhali uruhusu watumishi wako wakae huko Gosheni.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.