Native Bible

Genesis 43:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baada ya kunawa uso wake, akatoka nje na huku akijizuia akasema, “Pakueni chakula.”

Genesis 43:31 in English

Genesis 43:31 · Berean Standard Bible

Then he washed his face and came back out. Regaining his composure, he said, “Serve the meal.”

Context

29Alipotazama na kumwona Benyamini ndugu yake, mwana wa mama yake hasa, akauliza, “Je, huyu ndiye ndugu yenu wa mwisho, ambaye mlinieleza habari zake?” Ndipo akasema, “Mungu na akufadhili, mwanangu.” 30Akiwa ameguswa sana kwa kumwona ndugu yake, Yosefu akatoka nje kwa haraka na kutafuta mahali pa kulilia. Akaingia kwenye chumba chake cha pekee na kulilia humo. 31Baada ya kunawa uso wake, akatoka nje na huku akijizuia akasema, “Pakueni chakula.” 32Wakampakulia Yosefu peke yake, ndugu zake peke yao na Wamisri waliokula pamoja naye peke yao, kwa sababu Wamisri wasingeweza kula pamoja na Waebrania, kwa maana ilikuwa ni chukizo kwa Wamisri. 33Watu hao walikuwa wameketi mbele yake kwa mfuatano wa umri wao, kuanzia mzaliwa wa kwanza hadi mzaliwa wa mwisho, wakatazamana wao kwa wao kwa mshangao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.