Mwanzo 42:31
Genesis 42:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini tulimwambia, ‘Sisi ni watu waaminifu, sio wapelelezi.
Genesis 42:31 in English
Genesis 42:31 · Berean Standard Bible
But we told him, ‘We are honest men, not spies.
Context
29Walipofika kwa Yakobo baba yao katika nchi ya Kanaani, wakamweleza mambo yote yaliyowapata. Wakasema, 30“Huyo mtu ambaye ndiye bwana katika nchi hiyo alisema nasi kwa ukali, akatutendea kana kwamba sisi tulikuwa tunaipeleleza nchi. 31Lakini tulimwambia, ‘Sisi ni watu waaminifu, sio wapelelezi. 32Tulizaliwa ndugu kumi na wawili, wana wa baba mmoja. Mmoja alikufa, na mdogo wetu wa mwisho yupo na baba yetu huko Kanaani.’ 33“Ndipo huyo mtu aliye bwana katika nchi hiyo alipotuambia, ‘Hivi ndivyo nitafahamu kuwa ninyi ni watu waaminifu: Mwacheni mmoja wa ndugu zenu pamoja nami hapa, kisha nendeni mpeleke chakula kwa ajili ya jamaa yenu inayoteseka kwa njaa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.