Mwanzo 42:17
Genesis 42:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akawaweka wote chini ya ulinzi kwa siku tatu.
Genesis 42:17 in English
Genesis 42:17 · Berean Standard Bible
So Joseph imprisoned them for three days,
Context
15Na hivi ndivyo mtakavyojaribiwa: Hakika kama Farao aishivyo, hamtaondoka mahali hapa mpaka ndugu yenu mdogo aje hapa. 16Tumeni mmoja wenu akamlete huyo ndugu yenu, wengine mtawekwa gerezani, ili maneno yenu yajaribiwe kuona kama mnasema kweli. La sivyo, hakika kama Farao aishivyo ninyi ni wapelelezi!” 17Akawaweka wote chini ya ulinzi kwa siku tatu. 18Siku ya tatu Yosefu akawaambia, “Fanyeni hili nanyi mtaishi, kwa maana namwogopa Mungu: 19Ikiwa ninyi ni watu waaminifu, mmoja wa ndugu zenu na abaki kifungoni, nanyi wengine pelekeni nafaka kwa jamaa yenu wanaoteseka kwa njaa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.