Mwanzo 40:18
Genesis 40:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yosefu akamwambia, “Hii ndiyo maana yake: Vikapu vitatu ni siku tatu.
Genesis 40:18 in English
Genesis 40:18 · Berean Standard Bible
Joseph replied, “This is the interpretation: The three baskets are three days.
Context
16Yule mwokaji mkuu alipoona kuwa Yosefu amefasiri ikiwa na maana nzuri, akamwambia Yosefu, “Mimi pia niliota ndoto: Kichwani mwangu kulikuwepo vikapu vitatu vya mikate. 17Katika kikapu cha juu kulikuwa na aina zote za vyakula vilivyookwa kwa ajili ya Farao, lakini ndege walikuwa wakivila kutoka kwenye kikapu nilichokuwa nimebeba kichwani.” 18Yosefu akamwambia, “Hii ndiyo maana yake: Vikapu vitatu ni siku tatu. 19Katika siku hizi tatu, Farao atakata kichwa chako na kukutundika juu ya mti. Nao ndege watakula nyama ya mwili wako.” 20Mnamo siku ya tatu, ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Farao, naye akawaandalia maafisa wake wote karamu. Akawatoa gerezani mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu, akawaweka mbele ya maafisa wake:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.