Mwanzo 4:7
Genesis 4:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ukifanya lililo sawa, je, hutakubalika? Lakini usipofanya lililo sawa, dhambi inakuvizia mlangoni mwako, inakutamani wewe, lakini inakupasa uishinde.”
Genesis 4:7 in English
Genesis 4:7 · Berean Standard Bible
If you do what is right, will you not be accepted? But if you refuse to do what is right, sin is crouching at your door; it desires you,* but you must master it.”
Context
5lakini Mungu hakumkubali Kaini pamoja na sadaka yake. Kwa hiyo Kaini akakasirika sana, uso wake ukawa na huzuni. 6Kisha Bwana akamwambia Kaini, “Kwa nini umekasirika? Kwa nini uso wako una huzuni? 7Ukifanya lililo sawa, je, hutakubalika? Lakini usipofanya lililo sawa, dhambi inakuvizia mlangoni mwako, inakutamani wewe, lakini inakupasa uishinde.” 8Basi Kaini akamwambia ndugu yake Abeli, “Twende shambani.” Walipokuwa shambani, Kaini akamshambulia Abeli ndugu yake, akamuua. 9Kisha Bwana akamuuliza Kaini, “Ndugu yako Abeli yuko wapi?”
Akamjibu, “Sijui, je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.