Mwanzo 4:12
Genesis 4:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Utakapoilima ardhi, haitakupa tena mazao yake. Utakuwa mtu wa kutangatanga duniani asiye na utulivu.”
Genesis 4:12 in English
Genesis 4:12 · Berean Standard Bible
When you till the ground, it will no longer yield its produce to you. You will be a fugitive and a wanderer on the earth.”
Context
10Bwana akasema, “Umefanya nini? Sikiliza! Damu ya ndugu yako inanililia mimi kutoka ardhini. 11Sasa umelaaniwa na umehamishwa kutoka ardhi, ambayo imefungua kinywa chake na kupokea damu ya ndugu yako kutoka mkononi mwako. 12Utakapoilima ardhi, haitakupa tena mazao yake. Utakuwa mtu wa kutangatanga duniani asiye na utulivu.” 13Kaini akamwambia Bwana, “Adhabu yangu ni zaidi ya niwezavyo kustahimili. 14Leo unanifukuza kutoka nchi, nami nitafichwa mbali na uwepo wako. Nitakuwa mtu wa kutangatanga asiyetulia duniani na yeyote anionaye ataniua.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.