Mwanzo 37:5
Genesis 37:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yosefu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi.
Genesis 37:5 in English
Genesis 37:5 · Berean Standard Bible
Then Joseph had a dream, and when he told it to his brothers, they hated him even more.
Context
3Basi, Israeli akampenda Yosefu kuliko yeyote miongoni mwa kaka zake, kwani ni mwanawe wa uzeeni, akamshonea joho lililorembwa vizuri sana. 4Ndugu zake walipoona kwamba baba yao anampenda Yosefu kuliko yeyote mwingine miongoni mwao, walimchukia na hawakusema naye neno lolote jema. 5Yosefu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi. 6Akawaambia, “Sikilizeni ndoto niliyoota: 7Tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani, ghafula mganda wangu ukasimama wima, wakati miganda yenu ikiuzunguka na kuuinamia.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.