Mwanzo 37:11
Genesis 37:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndugu zake wakamwonea wivu, lakini baba yake akaliweka jambo hilo moyoni.
Genesis 37:11 in English
Genesis 37:11 · Berean Standard Bible
And his brothers were jealous of him, but his father kept in mind what he had said.
Context
9Kisha akaota ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake akisema, “Sikilizeni, nimeota ndoto nyingine, wakati huu jua, mwezi na nyota kumi na moja zilikuwa zinanisujudia.” 10Alipomwambia baba yake pamoja na ndugu zake, baba yake akamkemea akisema, “Ni ndoto gani hii uliyoota? Hivi kweli mama yako na mimi na ndugu zako tutakuja kukusujudia wewe hadi nchi?” 11Ndugu zake wakamwonea wivu, lakini baba yake akaliweka jambo hilo moyoni. 12Basi, ndugu zake walikuwa wamekwenda kuchunga makundi ya baba yao karibu na Shekemu, 13naye Israeli akamwambia Yosefu, “Kama ujuavyo, ndugu zako wanachunga makundi huko karibu na Shekemu. Njoo, nitakutuma kwao.”
Yosefu akajibu, “Vema sana, niko tayari.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.