Mwanzo 29:21
Genesis 29:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo Yakobo akamwambia Labani, “Nipe mke wangu. Muda wangu umekamilika, nami nataka nikutane naye kimwili.”
Genesis 29:21 in English
Genesis 29:21 · Berean Standard Bible
Finally Jacob said to Laban, “Grant me my wife, for my time is complete, and I want to sleep with her.”
Context
19Labani akasema, “Ni bora zaidi nikupe Raheli kuliko kumpa mtu mwingine yeyote. Kaa pamoja na mimi hapa.” 20Kwa hiyo Yakobo akatumika miaka saba ili kumpata Raheli, lakini ilionekana kwake kama siku chache tu kwa sababu ya upendo wake kwa Raheli. 21Ndipo Yakobo akamwambia Labani, “Nipe mke wangu. Muda wangu umekamilika, nami nataka nikutane naye kimwili.” 22Basi Labani akaalika watu wote wa mahali pale na akafanya karamu. 23Lakini ilipofika jioni, akamchukua Lea binti yake akampa Yakobo, naye Yakobo akakutana naye kimwili.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.