Mwanzo 27:20
Genesis 27:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Isaki akamuuliza mwanawe. “Umepataje haraka namna hii, mwanangu?” Akajibu, “Bwana Mungu wako amenifanikisha.”
Genesis 27:20 in English
Genesis 27:20 · Berean Standard Bible
But Isaac asked his son, “How did you ever find it so quickly, my son?” “Because the LORD your God brought it to me,” he replied.
Context
18Akamwendea baba yake akasema, “Baba yangu.”
Akajibu, “Naam, mwanangu, wewe ni nani?” 19Yakobo akamwambia baba yake, “Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza. Nimefanya kama ulivyoniambia. Tafadhali uketi, ule sehemu ya mawindo yangu ili uweze kunibariki.” 20Isaki akamuuliza mwanawe. “Umepataje haraka namna hii, mwanangu?”
Akajibu, “Bwana Mungu wako amenifanikisha.” 21Kisha Isaki akamwambia Yakobo, “Mwanangu tafadhali sogea karibu nami ili nikupapase, nione kama hakika ndiwe Esau mwanangu, au la.” 22Yakobo akasogea karibu na baba yake Isaki, ambaye alimpapasa na kusema, “Sauti ni ya Yakobo, bali mikono ni ya Esau.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.