Mwanzo 25:26
Genesis 25:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baadaye, ndugu yake akatoka, mkono wake ukiwa umemshika Esau kisigino; akaitwa jina lake Yakobo.* Isaki alikuwa mwenye miaka sitini Rebeka alipowazaa.
Genesis 25:26 in English
Genesis 25:26 · Berean Standard Bible
After this, his brother came out grasping Esau’s heel; so he was named Jacob.* And Isaac was sixty years old when the twins were born.
Context
24Wakati wake wa kujifungua ulipotimia, walikuwepo mapacha wa kiume tumboni mwake. 25Wa kwanza kuzaliwa alikuwa mwekundu, mwili wake wote ulikuwa kama mtu aliyevaa vazi lenye nywele; wakamwita jina lake Esau.* 26Baadaye, ndugu yake akatoka, mkono wake ukiwa umemshika Esau kisigino; akaitwa jina lake Yakobo.* Isaki alikuwa mwenye miaka sitini Rebeka alipowazaa. 27Watoto wakakua, naye Esau akakuwa mwindaji hodari, mtu wa mbugani, wakati Yakobo alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa nyumbani. 28Isaki, ambaye alikuwa anapendelea zaidi nyama za porini, alimpenda Esau, bali Rebeka alimpenda Yakobo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.