Mwanzo 25:20
Genesis 25:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Isaki alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomwoa Rebeka binti Bethueli Mwaramu kutoka Padan-Aramu, nduguye Labani Mwaramu.
Genesis 25:20 in English
Genesis 25:20 · Berean Standard Bible
and Isaac was forty years old when he married Rebekah, the daughter of Bethuel the Aramean from Paddan-aram * and the sister of Laban the Aramean.
Context
18Wazao wa Ishmaeli waliishi kuanzia nchi ya Havila hadi Shuri, karibu na mpaka wa Misri, unapoelekea Ashuru. Hao waliishi kwa uhasama na ndugu zao wote. 19Hivi ndivyo vizazi vya Isaki mwana wa Abrahamu.
Abrahamu akamzaa Isaki, 20Isaki alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomwoa Rebeka binti Bethueli Mwaramu kutoka Padan-Aramu, nduguye Labani Mwaramu. 21Isaki akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, kwa sababu alikuwa tasa. Bwana akajibu maombi yake na Rebeka mkewe akapata mimba. 22Watoto wakashindana tumboni mwake, akasema, “Kwa nini haya yanatokea kwangu?” Kwa hiyo akaenda kumuuliza Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.